Muungano wa vyama vya siasa nchini Ufaransa vya mrengo wa kulia unaoongozwa na rais wa zamani wa nchi hiyo, Nicolas Sarkozy unaonekana kuongoza katika uchaguzi wa tawala za mikoa katika duru ya kwanza. Matokeo ya awali yanaonyesha kuwa wahafidhina wa muungano wa UMP/UDI unaongoza kwa kati ya asilimia 29.7 na 32.5 ya kura zilizohesabiwa hadi sasa. Chama cha siasa kali za mrengo wa kulia cha Front National-FN, kinachoongozwa na Marine Le Pen kinapewa kati ya asilimia 24.5 na 26. Nacho chama cha Kisoshalisti cha Rais Francois Hollande kimeshika nafasi ya tatu baada ya kupata kati ya asilimia 19.7 na 25 ya kura.
23 Machi 2015 - 11:25
Msimbo wa Habari: 678511
Muungano wa vyama vya siasa nchini Ufaransa vya mrengo wa kulia unaoongozwa na rais wa zamani wa nchi hiyo